Tags

,

Siku nyingi tangu nikuone
Hapo Juba Sudan ya kusini
Na roho yanduda nikikuwaza
Mtoto wa Ethiopia wee
Ukarimu wako sitasahau milele
Ndo nakutumia barua pepe
Nikujulie hali

Barua pepe,
Naituma kwako wee
Njoo karibu ujumbe nikupe
Karibu na mbali upepee
Milima na mabonde uvuke
Ng’ambo ya bahari ya hindi ufike

Barua peleka salamu, kwa wangu muhibu
Ukifika kamwambie, Kwamba ninapata taabu
Na yeye ndiye wangu tabibu
Mtibabu, maradhi yangu kuyatibu
Majibu yake kwangu muhimu
Dawa tosha kwa yangu matibabu

Ninashauku ya jibu, nijibu nipate tua
Mzigo mzito unaonisumbua
Mpaka kizunguzungu chanizingua
Homa kali, na nyongo kuitapika
Fanya hima barua pepe kuiandika
Kabla pumzi hazijanishuka
Mate kunikauka, na roho kukatika

Shida yangu ni kukujulia hali, rafiki
Nataka jua kama bado nimo kwenye yako akili

http://profarmsconsultants.kbo.co.ke

Advertisements